Habari

ZIDANE ASEMA HANA WASIWASI NA RONALDO, ANAMWAMINIA

on

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine
Zidane amesema kuwa hana wasiwasi kuhusu kiwango cha straika wake, Cristiano
Ronaldo, baada ya Mreno huyo kushindwa kuziona nyavu katika mchezo wa usiku wa
kuamkia juzi ambao walikwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya Villarreal.
Ronaldo alikosa mechi ya Kombe
la UEFA Super Cup dhidi ya Sevilla na mechi mbili za La Liga kutokana na
majeraha ya goti ambayo aliyapata wakati wa fainali za mataifa ya Ulaya “Euro
2016”.
Lakini aliweza kurejea uwanjani
kati amchezo walioibuka na ushindi wa mabao 5-2dhidi ya Osasuna kabla ya
kuiongoza Real Madrid kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sporting CP katika
Ligi ya Mabingwa ambapo aliweza kufunga bao kila mechi.
Hata hivyo usiku wa kuamkia
juzi staa huyo mwenye umri wa miaka 31 hakuweza kuziona nyavu dhidi ya
Villareal ambapo Real Mdrid walipoteza pointi kwa mara ya kwanza na Zidane
anaona hana haja ya kuumia kichwa.
“Kutokana na ninavyomuheshimu
Cristiano, sina wasiwasi naye na pia ni mchezaji muhimu kwetu sisi dhidi ya
Villareal kama alivyo mara zote,” Zidane aliwaambia waandishi wa habari.

“Sina hofu asipofunga. Jambo la
muhimu ni kwamba yupo uwanjani anatupigania. Huwa ninakuwa na hofu anapokuwa
nje ya uwanja,” aliongeza kocha huyo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *