Habari

JURGEN KLOPP “AWAFUNDA” MASTAA WAKE KUTOHOFIA KUKAMIWA NA TIMU PINZANI

on

KOCHA wa Liverpool Jurgen Klopp
ni kama amewapa darasa nyota wake baada ya kusema kuwa wanatakiwa kutohofia
kukamiwa timu pinzani baada wamwisho wa wiki iliyopita kukutana na Southampon.
Katika mchezo wa Jumamosi
vijana hao wa Klopp walipata nafasi nyingi za kupachika mabao lakini wakajikuta
wakitoka suluhu kwenye uwanja wa St Mary hivyo kujikuta wakitupwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
Hata hivyo Mjerumani huyo
halalamiki kuhusu wenye kucheza soka kupaki basi dhidi ya timu ambayo ina uwezo
wa kufunga mabao ambayo wameshafunga 30 katika mechi 12 za Ligi hiyo.
“Haikuwa maana kuhofia hilo,” Klopp aliyaambia
magazeti ya Uingereza.
“Unaweza kuwaagiza waje mbele
na kutupa sisi nafasi ama kitu chochote,” aliongeza kocha huyo.

Alisema kuwa kabla msimu kuanza walifanyia
kazi jambo hilo na ndiyo maana anasema kuwa anajisikia mwenye furaha kwa
kiwango walichokionyesha dhidi ya Southampon kwa sababu wanaendelea kufanya
vizuri.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *