Habari

CHELSEA YAKWAA KISIKI KWA TOTTENHAM, YALAMBWA 2-0 …Dele Alli si mtu wa mchezo mchezo

on

MSHAMBULIAJI kinda wa Tottenham Spurs,  Dele Alli amesitisha mbio za Chelsea baada ya kuifungia timu yake mabao yote mawili yaliyoibua ushindi wa 2-0 katika mchezo mkali wa Premier League.
Kabla ya mchezo huu, Chelsea inayoongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano, ilikuwa imeshinda mechi 13 mfululizo za Premier League na kuzitia woga timu pinzani.
Alli alifunga bao la kwanza dakika ya 45 kabla ya kutupia la pili dakika ya 54 kwa mpira ulioanzia kwa Kyle Walker aliyempenyezea Christian Eriksen.
Eriksen akapiga krosi iliyomkuta  Alli akiwa katikati ya Victor Moses na Cesar Azpilicueta, lakini akawa mwepesi kwenda hewani na kukwamisha mpira wavuni kwa kichwa.
TOTTENHAM (3-4-3): Lloris 6.5; Dier 7, Alderweireld 7.5, Vertonghen 7; Walker 7, Wanyama 7, Dembele 7.5 (Winks 74, 6), Rose 7.5; Eriksen 8, Kane 6.5 (Son 90), Alli 8.5 (Sissoko 86, 6).
CHELSEA (3-4-3): Courtois 6; Azpilicueta 6, Luiz 6.5, Cahill 6; Moses 5.5 (Batshauyi 85, 6), Kante 6.5 (Fabregas 79, 6), Matic 6.5, Alonso 5.5 (Willian 65, 6); Pedro 6, Costa 6, Hazard 6.5

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *