Habari

SANTI CAZORLA “AIUMIZA” ARSENAL… haijulikani pengo lake litazibwa vipi

on

WAKATI Arsenal ikiwa na nafasi ngumu ya kutwaa ubingwa wa England, hivi
sasa kuna swali linaulizwa kuwa timu hiyo itaziba vipi pengo la kiungo wake
Santi Cazorla.
Cazorla alifanyiwa operesheni ya enka ya mguu wa kulia Desemba 7, mwaka
jana nchini Sweden na atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Kufuatia pengo lake timu hiyo imekuwa inasuasua na hivi karibuni ilipoteza
mechi mbili dhidi ya Everton na Manchester City na kuifanya kupoteza mwelekeo
wa kutwaa ubingwa.
Cazorla anaweza kuwa sio mchezaji bora lakini ni muhimu katika kikosi hicho
na hasa linapokuja suala la uchezeshaji wa timu.

Kiungo huyo anategemewa sana na Arsenal na hasa katika kumiliki mpira na
kuongoza mashambulizi ambapo kukosekana kwake kumeiathiri timu kwa kiasi
kikubwa.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *