Habari

HASSAN KABUNDA AFICHUA ALIVYOGOMA KUJIUNGA SIMBA NA KUAMUA KUTUA MWADUI

on

HASSAN Salum  Kabunda ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa
yanga, Salum Kabunda “Ninja”, amedai kuwa aliwahi kufuatwa mara kadhaa na watu
wa Simba ili ajiunge nao lakini akagoma na kuamua kuichezea timu ya Mwadui.
Kabunda ambaye mkataba wake na
Mwadui unamalizika mwishoni mwa msimu huu, alisema kwamba hakutaka kufanya maamuzi
ya kukurupuka kusaini mkataba wa Simba, lakini pia mama yake alikuwa chach ya
yeye kuwagomea wekundu hao wa Msimbazi.
“Mama alichangia mimi
kutokwenda Simba, lakini hata mimi pia sikutaka kukurupuka na kuingia mkataba
na Simba, niliona Mwadui pananifaa wakati huu,” alisema Kabunda.
“Mkataba wangu unamalizika
mwisho wa msimu huu na hakuna timu niliyofanya nayo mazungumzo isipokuwa pia
sioni ni kwa jinsi gani klabu yagu ya mwadui inaweza kuniacha,” aliongeza nyota
huyo.

Pamoja na hayo, nyota huyo
alidai kuwa maamuzi juu yahatima yake baada ya kumalika kwa msimu huu
yanategemea na namna ambavyo watakubaliana na uongozi wa klabu yake.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *