Habari

WIMBO “MOYO KAMA MACHO” WA KIVURANDE JUNIOR KUZINDULIWA MAISHA BASEMENT

on

UONGOZI wa klabu ya Maisha
Basement, Dar es Salaam uko katika mazungumzo na Mfalme wa Kibao Kata,
Kivurande Junior ili kumshawishi kufanyia klabuni hapo uzinduzi wa kibao chake
cha mduara cha “Moyo Kama Macho.”
Kibao “Moyo Kama Macho” ambacho
bado hakijaachiwa rasmi, kimeibuka kuwa gumzo kubwa hivi sasa kutokana na
mashabiki pamoja na wapenzi kukisubiri kwa hamu.
Akiongea na saluti5, Kivurande
amesema kuwa wako katika hatua ya mwisho ya mazungumzo na Maisha Basement
ambapo anaamini muda si mrefu mashabiki watatangaziwa tarehe ya uzinduzi wa
kibao hicho.
“Nawaomba mashabiki waendelee
kutuvuta subira ingawa nafahamu kwamba wana shauku na wimbo huo, mambo yanaendelea
kuwa sawa na wakati wowote tutawaeleza siku ya uzinduzi pale Maisha Basement,”
amesema Kivurande.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *