Habari

HUSSEIN MACHOZI AFICHUA SABABU YA KUINGIA LEBO YA MAN WATER

on

MSANII wa bongofleva, Hussein
Machozi mara nyingi hufanya kazi zake mwenyewe lakini kwa sasa ameamua kuwa
chini ya lebo ya Man Water katika kibao chake kinachokwenda kwa jina la ‘Nipe
Sikuachi’, katika studio ya Combination Sound.
Akiongea na mwandishi wetu jijini
Dar es Salaam jana, Hussein Machozi alielezea sababu zilizomfanya awe chini ya
usimamizi wa Man Water akisema: “Man Water kwanza anajua kufanya kazi na kila
kazi yake huwa inabamba sana, hajawahi kukosea, pili ni mshikaji wangu toka
kitambo.”
Msanii huyo  ameahidi kurudi kwa kishindo baada ya kupotea
kwa muda mrefu kwenye muziki aligusia kuwa yeye kama mwanamuziki hapendi
kujaribu hivyo atasimama kwa miguu yote miwili,na amewahakikishia mashabiki
wake kufanya kazi nzuri zadi.

Hussein Machozi ambae
anatambulika kwa nyimbo zake kali ikiwemo ‘Utaipenda’ na nyinginezo ambazo
zilichangia kumuweka juu na kumfanya awe na jina kubwa kwenye muziki.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *