Habari

MIRAJI ADAM AKACHA MECHI YA MAJARIBIO SINGIDA UNITED

on

BEKI wa zamani wa Simba, Miraji
Adam amempiga chenga ya mwili kocha wa Singida United Hans Pluijim baada ya
kushindwa kutokea katika majaribio ya kikosi, akihofia kuumia.
Miraji ambaye msimu uliopita
alikuwa katika kikosi cha African Lyon kilichoshuka daraja Ligi Kuu Tanzania
Bara, aligoma kufanyiwa majaribio ili baadae aweze kusajiliwa.
Akiongea jana, Katibu mkuu wa
timu hiyo Abdulhaman Sima alisema mchezaji huyo alitakiwa kuungana na wachezaji
wenzake katika mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Super Cup iliyomalizika juzi
kwenda uwanja wa uhuru, lakini hakutokea.
Sima alisema kuwa kocha wao,
Pluijim alitaka kumuangalia mchezaji huyo kwenye michuano hiyo ili kama
akilidhishwa na kiwango chake waweze kumsajili na kushindwa kutokea kwake ni
kama alikataa ofa yao.
“Miraji tulikuwa kwenye mazungumzo
nae ya Ligi Kuu Bara na Koch alitaka amuone kwenye michuano ya Super Cup
hakutokea tukaona kama alikataa,” alisema Sima.
Saluti5 ilimtafuta Miraji ili
aweze kuzungumzia suala hili, akasema yeye ni mchezaji na alitoka kwenye Ligi kwa
hiyo kiwango chake kinajulikana.
Miraji alisema, walichotaka
Singida United kumfanyia majaribio kwenye michuano ya Super Cup ni jambo ambalo
hakulitaka.

Alisema hakutaka kwenda
kuichezea timu hiyo kwenye michuano hiyo kwa hofu ya kuumia wakati hana mkataba
na klabu hiyo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *