Habari

MAVUGO AWASHAURI SIMBA KUACHANA NA BEKI WA LYON SPORT YA RWANDA

on

STRAIKA wa klabu ya Simba raia
wa Burundi Laudit Mavugo amewadokeza siri nzito viongozi wa klabu hiyo kwamba
waachane na suala la kumfuatilia beki wa Lyon Sport, Manzi Thierry akiamini
kuwa nyota huyo ana kiwango cha kawaida tofauti na mabeki wazawa.
Simba ilikuwa na mipango ya
kumleta beki huyo kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara pamoja na
michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Manzi ambaye yupo katika kikosi
cha taifa cha timu ya Rwanda, Amavubi amekuwa katika rada za Simba kwa ajili ya
kuinasa saini yake lakini ili kuimarisha safu yao ya ulinzi.
Mara baada ya kujiridhisha na
kiwango chake Simba imeamua kuachana na beki huyo na tayari inekuwa ni kama jambo linaloonekana kuwa neema kwa watani wao Yanga ambao wameanza kutupa ndoano kwa mlinzi huyo wa
kati.
Yanga tayari imeanza
mikakati hiyo baada ya kujiridhisha kwa kiwango alichokionyesha katika mechi
kati ya Taifa Stars na Rwanda iliyopingwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza.
Mavugo amesema kwamba anamfahamu vizuri Manzi kutokana na kuwahi kukutana nae mara kadhaa
wakiwa katika majukumu ya timu zao za taifa hivyo anaamini kwamba beki huyo ana
tofauti na mabeki wazawa.
Alisema anamfahamu vizuri
kutokana kucheza nae klabu moja nchini mwake na kusema kuwa ni beki mzuri lakini
bado anaamini kuna mabeki wazuri zaidi wa hapa nchini waliomzidi kiwango.
“Ni beki mzuri lakini
ukiangalia uwezo wake na mabeki wa hapa nchini ninaamini bado Tanzania kuna wenye uwezo mzuri ambao wanamzidi kiwango,”alisema.

Mavugo alisema ana imani na usajili
unaofanywa na uongozi wa klabu hiyo kwa kufanyia kazi mapungufu
yaliyojitokeza katika mechi za msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *