Habari

HAKUNA NAMNA!! HENRIKH MKHITARYAN AKUBALI KWENDA ARSENAL

on

HENRIKH MKHITARYAN
amekubali uhamisho wa kweda Arsenal, hii ni kwa mujibu wa mwandishi wa Armenia,
Thibaud Vezirian.
Kama ni kweli, hatua
hiyo itarahisisha safari ya Alexis Sanchez kutoka Arsenal kwenda Manchester
United.
Vezirian, mwandishi anayejiita “Mfalme
wa Armenia” amedai Mkhitaryan mwenye umri wa miaka 28 amekubali kwenda Arsenal.
United ambayo ilimnunua Mkhitaryan kwa pauni milioni 26 kiangazi cha
2016, pia itailipa Arsenal pauni milioni 35 ili kumpata Sanchez.

Mkhitaryan amepoteza nafasi kwenye
kikosi cha kwanza Old Trafford msimu na hivyo kwenda kwake Arsenal inaweza kuwa
hatua nzuri kwake ya kuokoa kiwango chake.
Inaaminika kuwa kimsingi, Sanchez ameshakubaliana na Manchester United lakini kilichokuwa kinachelewesha ni utashi wa Mkhitaryan wa kwenda Arsenal jambo ambalo ni moja ya masharti ya Arsenal kwa United.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *