Burudani

ALLY CHOCKY AFANYA BONGE LA ‘KOLABO’ NA BEKA FLEVA

on

Mwimbaji nyota wadansi, Ally Chocky ambaye mkataba wake ndani ya Twanga Pepeta unaisha rasmi mwishoni mwa mwezi huu, anaendelea kupika nyimbo mpya kali tayari kwa kuanza maisha mapya ya kujitegemea.

Chocky ameingia studio kuandaa ngoma moja matata kwa kumshirikisha staa wa bongo fleva Beka Fleva (Flavour).
Saluti5 ilibahatika kumnasa Ally Chocky na Beka Flavour katika studio za C9 wakitupia masauti ya hatari ndani ya kigongo hicho kipya.
Ally Chocky akaimbia Saluti5 kuwa wimbo huo ameupa jina la “Sikuachi” na utapasua anga mara tu ya video yake kukamilika.
“Nataka niachie audio na video kwa pamoja,” alisema Ally Chocky na kuongeza kuwa uchuajuaji wa
video utaanza ndani ya siku chache zijazo.
  Beka Flavour  na Ally Chocky
 Beka Flavour (kushoto) akiwa na Ally Chocky (kulia)  katika picha ya pamoja na producer wao C9
Ally Chocky  na  Beka Flavour wakifuatilia mwenendo wa kazi yao mpya

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *