Muziki

BEKA FLAVOUR ASEMA: ‘NAANZAJE KUKATAA WITO WA KUFANYA ‘KOLABO’ NA ALLY CHOCKY’

on

Staa wa bongo fleva aliyetamba na kundi la Yamoto Band, Beka Flavour, amesema ni furaha kubwa kwake kufanya wimbo wa kushirikishwa na gwiji Ally Chocky.

Beka Flavour ameshirikishwa na Ally Chocky kwenye wimbo “Sikuachi” ambao utaachiwa hewani wiki kadhaa zijazo.

Wimbo huo umerekodiwa katika studio za C9 chini ya producer C9 Kanjenje.

Alipoulizwa na Saluti5 alipokeaje wito wa Ally Chocky, Beka akasema alifurahi na hakusita hata kwa sekunde moja.

“Naanzaje kukataa wito wa Ally Chocky? Hawa ndiyo waimbaji ambao tumekuwa tukiwasikia tangu utotoni, wakatuvutia hadi na sisi kuamua kufuata nyayo zao,” alisema Beka Flavour.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *