Michezo

CHELSEA YAINGIA KWENYE VITA YA KUMSAJILI BEKI SAMUEL UMTITI WA BARCELONA

on

Imeripotiwa kuwa klabu ya Chelsea inajiandaa kumsajili beki wa kati wa Barcelona Samuel Umtiti ambaye anawaniwa kwa nguvu na Manchester United.

Ripoti kutoka Hispania zinadai beki huyo mwenye umri wa miaka 24 anataka maboresho ya mkataba wake Barcelona kama matunda ya kiwango chake bora alichokionyesha msimu huu.

Hata hivyo Barcelona haipo tayari kumpa mara mbili ya mshahara wake wa sasa huku Manchester United ikitajwa kuwa ipo tayari kufikia kipengele cha manunuzi cha pauni 53 kilichoko kwenye mkataba wake na mshahara mnono juu yake.

Gazeti la Don Balon la Hispania linaandika kuwa Chelsea imeingia katika mpango wa kusaka saini ya Umtiti ili kuimarisha safu yake ya ulinzi baada ya kupwaya kwa David Luiz na Gary Cahill.

 

 

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *