Muziki

CLOUDS FM ‘YAIFUNGIA KAZI’ SMART BAND YA TABORA

on

Kipindi cha Weekend Bonanza cha Clouds FM ambacho mara kwa mara huruka ‘live’ kutoka kwenye maonyesho ya bendi za muziki wa dansi, Jumamosi hii kinatarajiwa kuruka kutoka mjini Tabora kwenye show ya bendi mpya, Smart Band.

Kiongozi wa bendi hiyo J Four Sukari ameiambia Saluti5 kuwa Jumamosi hii Smart Band watakuwa na onyesho maalum kwenye ukumbi wao wa nyumbani – Inferno Club ambapo watakuwa na ugeni mkubwa kutoka Clouds FM na Clouds TV kupitia vipindi vya “Weekend Bonanza” na “Mamaland”.

“Tutakuwa ‘live’ kupitia Weekend Bonanza ya Clouds FM chini ya mtangazaji Khamis Dacota,” alisema J Four.

Weekend Bonanza inaruka kila Jumamosi kuanzia saa 4 usiku hadi 7 usiku.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *