Habari

GIORGIO CHIELLINI WA JUVENTUS AFICHUA SIRI YAO YA USHINDI DHIDI YA TOTTENHAM

on

Beki wa Juventus Giorgio
Chiellini amesema kuwa waliamini watashinda mchezo wao dhidi ya Totteham na
kwamba utulivu ndiyo siri ya mafanikio yao.
Juve imeichapa
Tottenham 2-1 na kutinga robo fainali ya Champions League kwa bao 4-3 kufuatia
sare ya 2-2 katika mchezo wa kwanza.
Akihojiwa baada ya mchezo huo, Chiellini akasema:
“Tottenham wana wachezaji wazuri, lakini wamekuwa wakiruhusu kushambuliwa
kirahisi, jambo lililofanya tuamini kuwa tutashinda mchezo huu.
“Hata baada ya
wao kutangulia, bado tuliamini tutashinda, tukacheza kwa utulivu na kwa umakini
na hatimaye tukaibuka na ushindi”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *