Michezo

HARRY KANE AONDOKA UWANJANI NA MAGONGO, MOHAMED SALAH SASA ASHINDWE MWENYEWE

on

Mshabuliaji kinara wa upachikaji mabao katika Premier League msimu huu Harry Kane, yupo katika nafasi hatarishi ya kupitwa kwenye mbio za kusaka kiatu cha dhahabu baada ya kuumia kifundo cha mguu kwenye mechi dhidi ya Bournemouth.

Kane aliumizwa na kipa wa Asmir Begovic katika dakika ya 34 wakati akiwa kwenye harakati za kufunga. Akatolewa na nafasi yake ikachukuliwa na Erik Lamela.

Licha ya Kane kuondoka uwanjani huku akitembelea magongo, kocha wa Tottenham, Pochettino amesema anaamini si tatizo kubwa sana ingawa wanalazimika kusubiri. “Tutafanya vipimo kwenye kifundo chake cha mguu ili kujua ukubwa wa tatizo,” alisema kocha huyo.

Kuumia huku kwa Kane kunafanana na namna alivyoumia mwaka jana na kukaa nje kwa mwezi mmoja. Kane aliwaambia marafiki zake baada ya mchezo kuwa maumivu yanashabihiana na yale ya mwaka jana.

Kane anaongoza kwa magoli magoli 24 akiwa amefungana na Mohamed Salah wa Liverpool mwenye idadi kama hiyo, huku Sergio Aguero wa Manchester City akifuatia kwa karibu na magoli yake 21.

Rekodi ya upachikaji mabao ya Salah inamuweka pazuri kutwaa kiatu cha dhahabu iwapo Kane atakosa hata nusu tu ya mechi nane zilizosalia kabla ya msimu kumalizika. Sergio Aguero pia yupo katika nafasi nzuri ya kuwapiku Kane na Salah.

Harry Kane akiondoka uwanjani kwa kutumia ‘mkongojo’

 

 

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *