Habari

HIVI NDIVYO ISHA MASHAUZI ALIVYOWEKA HESHIMA MOMBASA

on

Mwimbaji bora wa
kike wa taarab Isha Mashauzi “Queen of the best melodies” au Jike la Simba
ukipenda, ameweka heshima Mombasa, Kenya kupitia onyesho lake lililofanyika
Jumamosi iliyopita.
Katika onyesho
hilo Isha Mashauzi aliwasuuza roho mashabiki wake wa Kenya kupitia nyimbo zake
tamu zikiwemo “Nani Kama Mama” na “Nimpe Nani”.
Onyesho hilo
lililohudhuriwa na mashabiki kibao lilifanyika katika ukumbi wa Talentos Beach
Resort ulioko maeneo ya Likoni.
Waandaji wa
onyesho hilo wakaimbia Saluti5 kuwa hawakutegemea mapokeo makubwa kiasi hicho
kutokana na ukweli kuwa onyesho hilo liliandaliwa kwa muda mfupi sana ambapo
matangazo yake hayakuzidi siku saba.
 Mashabiki wa Mombasa wakicheza goma la Isha Mashauzi
 Isha Mashauzi jukwaani
Isha Mashauzi akimimina uhondo kwa wakazi wa Mombasa, Kenya

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *