Habari

J FOUR SUKARI AFUNGUKA: ‘SMART BAND SIO KUNDI LA NDONDO, NIMEONDOKA RASMI TOT PLUS’

on

J Four Sukari, mwimbaji na kiongozi wa bendi mpya – Smart Band- ya mjini Tabora, amefunguka kuwa kundi hilo ni rasmi na sio ndondo kama wengi wanavyodhani.

Akiongea na Saluti5 kwa njia ya simu, J Four akasema yeye yupo rasmi Smart Band na sio kwamba amekwenda kuzuga kisha achukue hamsini zake.

“Nipo Smart Band kwa miguu yote miwili, nimeondoka rasmi TOT Plus. Kwasasa mimi ni msanii wa Smart Band,” alifafanua J Four.

Smart Band ilizinduliwa rasmi tarehe 14 Februari huko Tabora huku ikiwa na wasanii wengi wa TOT akiwemo J Four mwenyewe, Juma Jerry “JJ”, Frank Kabatano, God Kanuti na fundi mitambo Kiroboto.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *