KHALID CHOKORAA ASEMA SI LAZIMA BENDI ZIBANANE DAR ES SALAAM, ADAI MORO NI SHWARI MAPACHA WATATU WANAKULA KIULAINI

on

Mwimbaji na mkurugenzi wa  Mapacha Watatu Original, Khalid Chokoraa, amesema mji wa Morogoro ni shwari na yeye na bendi yake wanakula kiulaini.

Mapacha Watatu imelihama jiji la Dar es Salaam na kwenda kuishi Morogoro ambapo imepokewa vizuri na kufanya iwe na show zisizopungua nne kwa wiki.

Baadhi ya kumbi inazopiga Mapacha Watatu mjini Morogoro kila wiki ni Nyamatandala, Airport Pub, Gem Stone Pub na Samaki Samaki.

Akiongea na Saluti5, Chokoraa alisema umefika wakati wa bendi kutawanyika na kusaka soko jipya mikoani badala ya kubanana Dar es Salaam na kugombea wateja wale wale.

 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *