Muziki

KIKAO MUHIMU KWA WANAMUZIKI WA DANSI JUMATANO 14/3/2018 SAA 5 ASUBUHI NDANI YA VIJANA SOCIAL HALL

on

Kampuni ya Smooth Vibes inayoshughulika na kazi ya kuibua na kukuza vipaji vya wasanii, Jumatano tarehe 14/3/2018 itakutana na wanamuziki wa dansi ili kujadili kwa pamoja namna na kuupandisha muziki wa dansi.

Meneja wa Smooth Vibes, Abdul Malick Anania Sangura (Junior Anania), ameiambia Saluti5 kuwa mkutano huo utafanyika Kinondoni jijini Dar es Salaam ndani ya Vijana Social Hall kuanzia saa 5 asubuhi.

Anania amesema lengo la mkutano huo ni kubadilishana mawazo na kupeana mbinu za kuufanya muziki huo upenye sokoni kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Tunaamini baada ya mkutano huu, sisi kama Smooth Vibes tutapata pa kuanzia na kwa hakika tutaurejesha juu muziki wa dansi,” alisema Anania.

Anania akaongeza: “Sisi binafsi tunajua baadhi ya vitu vinavyouangusha muziki dansi ikiwemo ukosefu wa mbinu mpya  na za kisasa za kunadi kazi na mapungufu kwa wasanii, bendi na nyimbo za dansi .

“Pamoja na hayo, Smooth Vibes tumeitisha mkutano huu ili tupate maoni ya wasanii wa dansi, tusikie kilio chao na tujue wao wana sababu zipi wanadhodhani zinawaangusha sokoni.

“Baada ya mkutano huu naamini tutaondoka na sababu za msingi kutoka kila upande na kitakochuafata ni utekelezaji wa kuupandisha tena muziki dansi. Naomba wanamuziki na wadau wa muziki wa dansi wafike kwa wingi kadri inavyowezekana”.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *