Muziki

KIMYA KINGI KINA MSHINDO …NYOSHI AKAMILISHA NYIMBO 10 MPYA ZA BENDI YAKE MPYA

on

Mwimbaji mahiri wa muziki wa dansi, Nyoshi el Saadat amefichua kuwa amekamilisha kurekodi jumla ya nyimbo 10 za bendi yake mpya ya Bogoss Musica.

Nyoshi “Sauti ya Simba” anayejulikana pia kama Rais wa Vijana, ameiambia Saluti5 kuwa kimya chake kitakuwa na kishindo kikubwa kwa namna alivyotengeneza nyimbo kali zenye ladha tofauti.

Nyoshi amekuwa kimya kwa miezi nane tangu alipojiengua FM Academia Juni 23 mwaka jana baada ya utumishi wake wa takriban miaka 20.

Licha ya Nyoshi kufichua kuwa amesajili bendi yake ya Bogoss, lakini hadi leo hii bado mashabiki hawajabahatika kuonja ladha kundi hilo.

“Ni kweli nipo kimya, ni kwasababu sitaki kukurupuka, sitaki kuingiza kazi mbovu sokoni,” anaeleza Nyoshi.

Mwimbaji huyo anasema kazi inayofuata sasa ni kuandaa angalau video mbili kati ya hizo nyimbo kumi na kisha kuziachia hewani sambamba na utambulisho wa bendi utakaofanyika mwishoni mwa mwezi April.

Bogoss inaundwa na damu mchanganyiko – wapiga ala wazoefu, waimbaji chipukizi.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *