Habari

KING BLAISE ‘MFALME WA MARAIS’ AWEKA NGUVU ZAKE KWENYE ALBAM YAKE MPYA …nyimbo sita zilizokwenda shule

on

Mwimbaji na mtunzi mahiri King Blaise anayejipapambanua kama Mfalme wa Marais yuko mbioni kuachia albam yake mpya.

Hii itakuwa ni ‘project’ binafsi nje ya bendi ambapo King Blaise ameiambia Saluti5 kuwa albam hiyo itaundwa na nyimbo sita kali.

King Blaise amezitaja baadhi ya nyimbo kuwa ni pamoja na “Tunda” na “Naseku”.

“Nimeziandaa nyimbo hizi kwa umakini mkubwa na kwa kuzingatia mahitaji ya soko, watu wake mkao wa kula mambo mazuri yanakuja,” alisema King Blaise ambaye amekuwa
akizitumikia bendi za East Africa Ngwasuma ya Arusha na FM Academia ya jijini Dar es Salaam.

King Blaise amesema nyimbo zote sita zimekamilika kwa upande wa audio na sasa anaendelea kuzifanyia video.

“Nikishakamilisha video ya albam nzima, nitatambulisha baadhi ya nyimbo mwezi Mei mwaka huu,”alifafanua King Blaise.

 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *