Michezo

LIGI YAFIKIA PATAMU, YANGA YAANZA KUNYOA SHARUBU ZA SIMBA

on

Yanga SC ambayo imekuwa ikifukuza ‘mwizi’ kimya kimya, hatimaye imefanikiwa kulingana pointi na Simba baada ya kuichapa Stand United 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Hadi mapumziko Yanga ilikuwa ikiongoza 2-0 kwa magoli yaliyofungwa na Ally Ally (aliyejifunga) na Ibrahim Ajib katika dakika ya 7 na 11.

Kipindi cha pili kilijaa ushindani zaidi na ilichukua hadi dakika 84 nyavu kutikisika tena baada ya Tariq Seif kuifungia Stand United bao la pekee.

Hata hivyo iliwachukua Yanga dakika moja tu kuzima matumani ya Stand pale Obrey Chirwa alipofunga bao la tatu dakika ya 84 akimalizia kazi nzuri ya Said Juma “Makapu”.

Kwa matokeo hayo, Yanga iliyocheza mechi 21, imejikusanyia pointi 46 sawa na Simba.

Ingawa Simba ina kiporo cha mchezo mmoja, lakini tayari hofu na mashaka imeanza kutanda Msimbazi juu juu ya utawala wao kileleni mwa msimamo wa ligi.

Msimu uliopita licha ya Simba kuongoza ligi karibu msimu mzima, lakini Yanga iliyocharuka mwishoni na kutwaa ubingwa.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *