Michezo

MANCHESTER CITY YANUSA TAJI LA PREMIER LEAGUE …David Silva aiangamiza Stoke City

on

Manchester City imezidi kuukaribia ubingwa wa Premier League baada ya kuichapa Stoke City 2-0 kwenye uwanja wa Bet365, shujaa akiwa ni kiungo David Silva.

Kwa ushindi huo Man City imefikisha pointi 81 huku ikiwa imesalia michezo nane ligi kufikia ukingoni.

Kikosi cha Pep Guaridiola kinahitaji kushinda michezo mitatu tu ili kufikisha pointi 90 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote ile.

Akiwa katikati ya mabeki wawili, David Silva akafunga bao la kwanza la Man City katika dakika ya 10 akimalizia krosi ya Raheem Sterling kutoka wingi ya kulia.

Silva akaifungia Man City bao la pili dakika ya 4 tu ndani ya kipindi cha pili baada gonga nyingi zilizoishia kwa Jesus ambaye alitoa pasi ya mwisho kwa mfungaji.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *