Michezo

MANCHESTER UNITED YAAGA CHAMPIONS LEAGUE, YACHAPWA NA SEVILLA 2-1 OLD TRAFFORD … Roma yatinga robo fainali

on

Wissam Ben Yedder akitokea benchi  anaingia uwanjani dakika ya 72 na kwenda kubadili sura ya mchezo kwa kufunga mabao mawili ya haraka haraka baada ya kudumu mchezoni kwa dakika nane tu.

Naam! Manchester United imeaga michuano ya Champions League baada ya kufungwa na Sevilla 2-1 kwenye uwanja wa Old Trafford.

Timu hizo zilitoka sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza ulichezwa Hispania wiki tatu zilizopita. Sevilla inakwenda robo fainali.

Kiujumla Manchester United ilicheza soka bovu huku Sevilla ikicheza kwa malengo na kuudhiti eneo la kiungo.

Pengine kocha Jose Mourinho alifanya makosa kuamini kuwa  amemaliza kazi kwa sare ya bila magoli ugenini na hivyo kuifanya timu yake icheze kwa kujihami Old Trafford huku ikisaka magoli kwa mashambulizi ya kushtukiza.

Wissam Ben Yedder alifunga mabao ya Sevilla  katika dakika ya 74 na 78 wakati lile la United lilifungwa na Romelu Lukaku dakika ya 84.

Dakika ya 90 Wissam Ben Yedder angeweza kufunga bao lake la tatu baada ya kuwalaghai mabeki wa United na kubaki yeye na De Gea lakini shuti lake likapanguliwa kwa mguu na mlinda mlango huyo wa kimataifa wa Hispania.

Katika mchezo mwingine wa 16 bora, Roma ya Italia imetinga robo fainali baada ya kuinyuka Shakhtar Donetsk 1-0, kama iliyofanya kwenye mchezo wao kwanza ambapo ilishinda pia 1-0.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *