Michezo

MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED WATAKA JOSE MOURINHO ATIMULIWE

on

Mashabiki wa Manchester United wametaka kocha Jose Mourinho ATIMULIWE kufuatia aibu ya kutolewa kwenye hatua ya 16 bora ya Champions League kwa kufungwa 2-1 na Sevilla kwenye uwanja wa nyumbani – Old Trafford.

United haijawahi kuvuka hatua hiyo tangu mwaka 2014 ambapo Jose Mourinho mwenye kikosi cha wachezaji ghali, aliaminika kuwa mtu sahihi wa kurejesha heshima ya klabu hiyo katika Champions League.

Daily Star la Uingereza linaandika kuwa mashabiki kibao wa Manchester United kupitia mitandao ya kijamii wametaka Mourinho afukuzwe.

Mourinho amekuwa na mahusiano mabaya na mashabiki wa Manchester United hususan wanaohudhuria mechi zinazochezwa Old Trafford na mara kadhaa amekuwa akizomewa kwa baadhi ya maamuzi yake.

Mmoja wa mashabiki hao ameandika: “Bado mtaendelea kumpa Mourinho mamilioni ya kusajili?@ManUtd. Hamuwezi kuona kuwa hana dira. Ni kweli Louis Van Gaal hajatufundisha kitu? Onyesheni nia ya dhati ya kumtimua. Sio mtu sahihi kwa klabu.

Mwingine akaandika: “Tafadhali fukuza Mourinho …mbinu zake ni mbaya kwa hadhi ya Man United.”

Baadhi ya maoni ya mashabiki wa Manchester United wanaotaka Mourinho afukuzwe

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *