Michezo

MOURINHO ASEMA LUKAKU NI SHUJAA WA TIMU HATA ASIPOFUNGA MAGOLI

on

Kocha Jose Mourinho wa Manchester United amesema mshambuliaji Romelu Lukaku ana mchango mkubwa sana kwenye timu na ndio maana anamkubali hata pale anapokuwa na ukame wa kupachika mpira wavuni.

Mourihno amesema hajali lolote pale linapokuja suala la Lukaku kutofunga mabao na kwamba anachoangalia ni mchango wake anaoutoa uwanjani.

Lukaku alitengeneza mabao yote mawili mawili yaliyofungwa na Marcus Rashford katika ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Livepool Jumamosi mchana.

“Mtazame anavyozunguka uwanjani, nafasi anazozitengeneza, angalia namna anavyosaidia timu pale wapinzani wanapopiga mipira ya kona,” alisema Mourinho.

 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *