Michezo

MOURINHO ASEMA MAN UNITED KUTOLEWA ULAYA MBONA KAWAIDA TU, ADA HATA YEYE ALISHATIOA MARA MBILI

on

Kocha Jose Mourinho ameongea kitu ambacho kinaweza kikazidi kuwachafua mashabiki wa Manchester United baada ya kutolewa na Sevilla katika hatua  16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

United jana usiku ilicheza soka bovu na kuchapwa 2-1 katika uwanja wa Old Trafford na kuaga mashindano kufuatia sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Hispania wiki tatu zilizopita.

Mara baada ya mechi hiyo kumalizika, Mourinho akasema haoni cha ajabu kutolewa kwa Manchester United na hiyo si mara ya kwanza kwa klabu hiyo kutupwa nje kwenye hatua za ‘knock out’.

Akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari ndani ya Old Trafford, Mourinho akasema: “Nilikaa kwenye kiti hiki kuongea na waandishi baada ya kuitoa Manchester United mara mbili kwenye Champions League. Niliitoa nikiwa na Porto, nilikaa hapa baada ya kuitoa  nikiwa na Real Madrid.

“Kwahiyo si jambo la ajabu kwa klabu hii kutolewa, ni kitu cha kawaida. Si jambo jipya”.

Manager Jose Mourinho has suggested Manchester United's last-16 exit is 'nothing new'

Mourinho made a first major mark on the European stage with a win at Old Trafford with Porto

 

 

 

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *