Michezo

MOURINHO HAPEPESAGI MACHO, AWAPASHA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED

on

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amewacharukia mashabiki wa klabu hiyo waliozomea baadhi ya maamuzi yake sambaba na kumzomea kiungo kiungo Scott McTominay.

Mashabiki wa United ndani ya Old Trafford walizomea maamuzi ya Mounrinho kumtoa Rashford na kumwingiza Fellaini kwenye mchezo dhidi ya Liverpool Jumamosi mchana.

Rashford ndiye aliyefunga magoli yote mawili katika mechi hiyo ambayo United iliibuka na ushindi wa 2-1.

Lakini pia mashabiki hao walikuwa wakimzomea Scott McTominay kila alipokuwa akirudisha mpira nyuma badala ya kupeleka mbele.

Mourinho amewashangaa  mashabiki hao na kusema aina hiyo ya ushabiki inaweza ikavunja ari ya wachezaji.

Mourinho anasema: “Nilimtoa Rashford kwasababu ya kumwepusha na kadi nyekundu, tayari alikuwa na kadi ya njano.

“Wakati wa mapumziko niliambiwa mchambuzi Garry Neville  alikuwa akihoji kwanini Rashford hakulimwa kadi nyekundu, uchambuzi ule ungeweza kuathiri mwenendo wa mwamuzi kama angesikia maneno ya Neville wakati wa mapumziko.

“Scott McTominay ni mchezaji mzuri na alikuwa anafanya vitu vingi ambavyo wachezaji wakubwa hawezi kuvifanya.  Wakati mwingine mashabiki ni watu wa ajabu sana”.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *