Michezo

PETR CECH ATIMIZA MECHI 200 BILA KUFUNGWA (CLEAN SHEETS) PREMIER LEAGUE …wa kuifikia rekodi hiyo ‘bado hajazaliwa’

on

Kipa Petr Cech wa Arsenal amefikisha mechi 20o bila kufungwa (clean sheets) katika Premier League, rekodi ambayo itachukua miaka mingi sana kuvunjwa.

Asrsenal imeichapa Watford 3-0 kwenye uwanja wa Emirates huku Cech mwenye umri wa miaka 35 akipangua penalti ya Troy Deeney.

Akizungumzia juu ya ‘clean sheet’ yake ya 200, Cech akaiambia Sky Sports: “Ni hatua ya ajabu. Ilituchukua mechi 18 kupata clean sheet tisa mwanzoni mwa msimu  nikafikisha 199 lakini ikanichukua mechi 11 kupata clean sheet ya 200.”

Mechi hiyo dhidi ya Watford ilikuwa ni clean sheet ya 38 kwa Cech akiwa na Arsenal katika Premier League. Zingine 162 alizipata akiwa na Chelsea.

Makipa wote wanaounda ‘top ten’ ya clean sheets katika Premier League hawapo tena kwenye ligi hiyo na wengi wao wameshastaafu, hatua itakayomfanya Petr Cech ashikilie rekodi hiyo kwa miaka mingi ijayo.

MAKIPA WANAONGOZA KWA ‘CLEAN SHEETS’ KATIKA PREMIER LEAGUE

1. Petr Cech – 200

2. David James – 169

3. Mark Schwarzer – 151

4. David Seaman – 140

5. Nigel Martyn – 137

6. Pepe Reina – 134

7. Edwin van der Sar – 132

8. Tim Howard – 132

9. Brad Friedel – 132

10. Peter Schmeichel – 128

 

 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *