Muziki

PICHA 7 ZA VICKING’S NIGHT: PAPII KOCHA NA NGUZA WASHINDWA KUJA NA ‘ONYESHO SHAWISHI’

on

Kwa mara ya kwanza Jumamosi usiku, Papii Kocha na baba yake Nguza Vicking, walifanya onyesho la kwanza la kibiashara ndani ya ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam. Onyesho likapewa jina la Vicking’s Night.

Wasanii hao walikuwa wakisubiriwa kwa hamu kubwa baada ya mashabiki wao kuwakosa kwa miaka 13 waliyokuwa jela wakitumikia adhabu ya kifungo cha maisha kabla ya kuachiwa kwa msamaha wa Rais Magufuli Disemba mwaka jana.

Hata hivyo, licha ya maandalizi mazuri ya onyesho hilo la kipekee, Papii na Nguza walipiga show ya kawaida sana.

Haikuwa show inayoshawishi kuwatafuta tena wasanii hao kwa kiingilio kile cha shilingi elfu ishirini hadi laki moja. Naam haikuwa ‘Show Shawishi’.

Ubora wa onyesho hilo unazungumzika zaidi kwa namna mastaa kibao walivyotinga ukumbini, hadhi ya ukumbi na nakshi nakshi zilizopamba ukumbi, lakini kamwe si kwa uzuri utumbuizaji wa Papii na Nguza.

Papii na Nguza walishindwa kuchangamka jukwaani, walishindwa kuwatia kiwewe mashabiki, walishindwa kushambulia jukwaa wao pamoja na waimbaji wao.

Kimahesabu, Q Chillah ambaye aliibuka jukwaani kusalimia kisanii, ndiye aliyeiteka show kwa kushangiliwa kwa nguvu na kunyanyua watu wengi kwenye viti vyao.

Hata kimavazi, wasanii wa Papii na Nguza hususan waimbaji, hawakuwa na yale mavazi yanayolingana na thamani ya show, walipiga pamba za kawaida zisizotosha kuiba jicho la mtazamaji kwa muda mrefu.

Kwa mtu anayekumbuka lile onyesho la Diamond Platnumz na timu yake nzima ya WCB pale Jangwani Sea Breeze Disemba mwaka juzi, ataelewa vizuri maana halisi ya ‘show shawishi’ kuanzia utumbuizaji hadi mavazi.

Pamoja na mapungufu hayo, Vicking’s Night linakuwa moja kati ya maonyesho makubwa yanayowahusu wasanii wa muziki wa dansi.

Mastaa kibao walikuwepo katika onyesho la Papii na baba yake

Q Chilla jukwaani

Papii Kocha akiimba mbele ya mashabiki wake

Bibie unayemuona hapo jukwaani ni mtoto wa Papii Kocha ambaye wakati baba yake anakwenda jela binti huyu alikuwa na miaka minne

Papii Kocha akiimba katika Vicking’s Night

Nguza Vicking akingurumisha gitaa

Taswira ya ukumbi wa King Solom katika Vicking’s Night

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *