Habari

PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG ATAJA KINACHOMFANYA ACHELEWE KUIZOEA STAILI YA ARSENAL

on

Licha Pierre-Emerick Aubameyang kuendelea kuipatia mabao muhimu Arsenal, lakini mshambuliaji huyo ametoa sababu inayomfanya achelewe kuifahamu vema staili ya uchezaji ya timu yake hiyo mpya.

Mshambuliaji huyo anaitaja sababu hiyo kuwa ni ile hali ya kutoshiriki mechi za Europa League, hatua  inayomnyima nafasi ya kucheza mechi ambazo zingemsaidia kuizoea timu haraka.

Aubameyang aliyetua Arsenal siku ya mwisho ya dirisha la usajili la mwezi Januari akitokea Borussia Dortmund kwa usajili wa pauni milioni 56 iliyovunja rekodi ya klabu, haruhusiwi kucheza Europa League

Nyota huyo alishashiriki michuano ya Ulaya akiwa na Dortmund ambayo nayo sasa inashiriki Europa League baada ya kushika nafasi tatu kwenye hatua ya makundi ya Champions League, jambo linamfanya Aubameyang asiruhisiwe kuitumikia Arsenal.

“Nakosa fursa ya kucheza kila baada ya siku tatu,” anaeleza Aubameyang mwenye umri wa miaka 28.

“Nilipokuwa Ujerumani nilikuwa nacheza mechi tatu kila baada ya siku tatu lakini sasa nacheza mara moja kwa wiki, nakosa nafasi ya kuizoea timu kwa haraka. Sijui nisemeje kwa Kiingereza lakini nimesikitika sana kwasababu nashindwa kuisadia timu yangu kwenye michuano hiyo. Hizi sheria zinanichanganya sana.” alisema Aubameyang.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *