Michezo

RASHFORD ‘AZUA’ BALAA, MOURINHO AMCHAMBA FRANK DE BOER

on

Jose Mourinho ameendelea kuonyesha kuwa ni mtu asiyependa ‘kuguswa’ baada ya kuanzisha mashambulizi makali kwa kocha wa zamani wa Crystal Palace, Frank De Boer.

Baada ya United kuishindilia Liverpool 2-1 huku magoli yote mawili yakifungwa Marcus Rashford, ndipo De Boer alipotoa maoni yaliyomchukiza Mourinho.

Kocha huyo za zamani wa Crystal Palace  akasema inahuzunisha Rashford kucheza chini Jose Mounrinho.

Alipoulizwa juu ya Rashford kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Sevilla, Mourinho akasema: “Nimesoma maoni kutoka kwa kocha mbovu kuliko wote katika historia ya Premier League – Frank De Boer.

“Anasema sio jambo jema kwa Rashford kuwa na kocha kama kwa sababu kitu muhimu kwangu ni ushindi. Nadhani kama Rashford angekuwa anafundishwa na Frank angejifunza kushindwa kwasababu alikuwa anashindwa kila mchezo.

“Najaribu kufanya kila lililo bora kwa kinda huyu. Kwa dhati nawapa pongezi watu wa academy ya klabu kwa kuvumbua na kukikuza kipaji chake. Nampongeza Louis Van Gaal ambaye alimwibua katika msimu wake wa kwanza.

“Lakini kama utaenda na takwimu halisi na kuangalia ni mechi ngapi amecheza chini yangu msimu huu na uliopita, bila shaka yoyote nitasema kuwa Rashford yupo katika ‘top five’ ya wachezaji wa United waliocheza mechi nyingi”.

Frank De Boer aliyefukuzwa Crystal Palace mwezi Septemba baada ya siku 77 huku akiwa ameiongoza timu katika michezo mitano ya Premier League na kufungwa mechi zote.

The former Crystal Palace manager said it’s ‘a pity’ that Marcus Rashford plays under Mourinho

 

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *