Michezo

VIDEO: CARRAGHER ALIVYOMTEMEA MATE MTOTO WA MIAKA 14 BAADA MAN UNITED KUICHAPA LIVERPOOL … AFUNGIWA KUCHAMBUA MECHI

on

Mchambuzi wa soka Jamie Carragher amefungiwa na Sky Sports baada ya kuonekana akimtemea mate mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14.

Carragher beki wa zamani wa Liverpool, alifanya tukio hilo la aibu baada ya mchezo wa Manchester United na Liverpool Jumamosi iliyopita ambapo timu yake ya zamani ilichapwa 2-1.

Tukio lilianza kwa baba shabiki wa United kumkejeli Caragher kwa kumtakia 2-1, 2-1 hali iliyomchukiza mchambuzi huyo na kutema mate kupitia dirisha la gari lake na mate yake yakaenda usoni mwa mtoto aliyekuwa amekaa kiti cha abiria katika gari la baba yake mnazi wa Mashetani Wekundu.

Carragher aliomba radhi ‘live’ kupitia Sky News Jumatatu, lakini bado akala kibano cha kusimamishwa kazi  ya kuchambua mchezo wa Stoke na Manchester City Jumatatu usiku huku hatma ya kibarua chake kinachomwingizia pauni milioni moja kwa mwaka, ikitarajiwa kujulikana hapo baadae.

Mbali na kusimamishwa na Sky Sports, Carragher pia amesimamishwa na Danish TV juu ya mchezo wa Champions League wiki hii kati ya Manchester United na Sevilla.

 Jamie Carragher afungiwa

Carragher told Sarah Hewson he had a 'moment of madness' and that it was 'disgusting'

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *