Muziki

CHRISTIAN BELLA AINGIA STUDIO KUACHIA ‘KOLABO’ NA WERRASON

on

Kwa mara nyingine tena Christian Bella ameendelea kudhihirisha kuwa yeye ndiye kinara wa kupeperusha bendera ya muziki wa dansi wa Tanzania kwa kupiga ‘kolabo’ na wasanii nyota wa Afrika, safari hii amemalizana na Werrason.

Naam, leo hii Bella ameingia studio kufanya wimbo wa pamoja na Werrason, hii ikiwa ni baada ya kufanya kolabo na mastaa wengine wa Afrika kama vile Koffi Olomide na J Martin.

Bella na Werrason wameifanya kazi hiyo katika studio za Kingodom zilizoko Sinza jijini Dar es Salaam.

Bella ameiambia Saluti5 kuwa wimbo huo ambao Werrason ameimba vipande vyake kwa lugha ya Kiswahili, utaachiwa muda si mrefu mara tu baada ya video kukamilika.

Bella ndiye msanii pekee wa dansi ambaye nyimbo zake zinatamba kwenye channel za kimataifa kama vile MTV na nyinginezo na hii inakuwa karata yake nyingine ya kujitanua kimataifa.

Bella na Werrason ndani ya studio za Kingdom

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *