Michezo

MOURINHO ATOA LA MOYONI KUHUSU POGBA

on

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema kiwango cha kiungo Paul Pogba kingekuwa endelevu kama angekuwa anajituma mazoezini.

Mourinho amefichua kuwa ubora aliouonyesha Pogba kwenye mchezo dhidi ya Manchester City ni matokeo ya kujituma mazoezini, jambo ambapo katika wiki kadhaa lilikuwa adimu kwa nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa.

Mourinho amesema: “Hiyo ni changamoto ambayo anatakiwa aikabili mwenyewe. Ni mchezaji mzuri sana lakini ubora wake ungeimarika kwa kujituma kwake mazoezini.

“Kwa wiki chache zilizopita amekuwa akifanya vizuri sana mazoezini, nina furaha sana kwake. Anapaswa kuendelea hivyo”.

 

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *