Habari

MPIGA SOLO RAMA KARENGA WA TOT AFARIKI DUNIA

on

Mpiga gitaa mahiri wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT) Rama Karenga  (pichani) amefariki dunia leo asubuhi.

Rama Karenga ambaye ni bingwa wa kucharaza solo gitaa, amefia katika hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa siku tatu kwa ugonjwa wa TB ya mapafu ambao ulikuwa ukimsumbua kwa wiki kadhaa.

Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini ameithibitishia Saluti5 kuwa Rama amefariki leo saa 12 aubuhi.

Tumaini amesema mipango ya mazishi inasubiri muongozo wa ndugu wa marehemu na kwamba taarifa itatolewa hapo baadae.

Rama Karenga anaacha pengo kubwa kwa tasnia ya muziki wa dansi na taarab, si kwa TOT tu bali hata kwa vikundi vingine ambapo mchango wake ulitumika.

Moja ya kazi bora aliyoifanya nje ya TOT ni kupitia wimbo wa “Sura Surambi” wa Mashauzi Classic ambapo humo marehemu Rama Karenga alipiga solo lililokwenda shule.

Rama ni mtoto wa gwiji wa muziki Shem Karenga ambaye alifariki miaka micheche iliyopita.

Rama pia ni kaka wa mwimbaji na rapa wa muziki wa dansi Mussa Karenga.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *