Habari

NYOSHI ASEMA HARUDI FM ACADEMIA LICHA YA KUOMBWA MSAMAHA

on

Nyoshi el Saadat ambaye kwasasa anajipanga kutoka na bendi yake mpya ya Bogoss Musica, amesema kamwe hawezi kurejea FM Academia licha ya ‘wamiliki’ kumuomba radhi.

Nyoshi alijiengua FM Academia aliyoitumikia kwa takriban miaka 20 baada ya kuvuliwa cheo cha urais wa bendi ambacho kilihamishiwa kwa Patcho Mwamba.

Waliofanya hivyo ni watoto wa aliyekuwa mmiliki wa bendi hiyo marehemu Martin Kasyanju.

Akiongea na kipindi cha Joto la Asubuhi cha EFM siku ya Ijumaa, Nyoshi akasema watoto hao wamemuomba radhi baada ya kugundua kuwa walifanya kosa  kumvunjia heshima kwa sababu ya chuki zilizopandikizwa na watu wasioitakia mema bendi.

Alipoulizwa iwapo yupo tayari kurejea FM Academia baada ya kuombwa radhi, Nyoshi akasema hana kabisa mpango huo.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *