Muziki

TWANGA PEPETA WAANDAA PARTY YA KUAGANA NA ALLY CHOCKY

on

Bendi ya The African Stars “Twanga Pepeta” imeandaa ‘party’ ya kuagana na mwimbaji nyota wa dansi Ally Chocky ambaye mkataba wake wa kuitumikia bendi hiyo ulifikia kikomo April Mosi.

Hii inakuwa ni hatua ya amani zaidi kufanyika baina ya pande hizo mbili.

Chocky anaachana na Twanga Pepeta kwa mara ya tatu ambapo mara mbili zilizopita, aliondoka kwa ‘gia’ kubwa na kuzua bifu la kufa mtu.

Katika vipindi hivyo, ilifikia wakati mwimbaji huyo alitoa wito kuwa siku akifa basi bosi wa Twanga Pepeta Asha Baraka asifike kwenye msiba wake.

Lakini safari hii Chocky anaachana vizuri na Twanga Pepeta na ameandaliwa onyesho maalum la kuagana na mashabiki wa Twanga Jumamosi ya April 28.

Onyesho hilo litafanyika The Jonz, Magomeni Mwembechai.

Asha Baraka ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo litapambwa na red carpet ya nguvu ambapo mashabiki watapata uwanja mpana wa kupiga picha za kumbukumbu kwa tukio hilo la kipekee.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *